Ufafanuzi juu ya risiti za mashine, kuna watu hawaoni umuhimu wake na hawajui kuwa kama hujapata hiyo risiti unakuwa umejizurumu mwenyewe.
Ipo hivi chukua bei halisi ya bidhaa iwe Tsh. X bila ya kodi (ambayo wewe ambaye hujapata hiyo risiti ya mashine inatakiwa uitoe kama risiti hujapewa)
Risiti inakujaje?
Kodi ya serikali ni 18% ya X.
Kwa hiyo Tsh. 0.18X ndio kodi.
Unaibiwaje kama hujachukua risiti?
Ukihitaji risiti manake inatakiwa ulipe Tsh. X+0.18X = Tsh. 1.18X
Kama risiti hujapewa inatakiwa ulipe Tsh. X tu.
Kwa lugha nyepesi, mfano bidhaa unayotakiwa kulipia Tsh. 100,000 usipo pewa risiti ina maana 18% ya kodi kwenye bei halisi X utakuwa unijidhurumu.
Ipo hivi X+0.18X=100,000
1.18X=100,000
X=84,746
Ina maana kodi ni 0.18X=0.18(84,746)= Tsh. 15,254 (usipo chukua risiti hii hela haina maana ya kuitoa inatosha Tsh. 84,746)